Leo ni siku ya kuzaliwa Sensei Rumadha Fundi (Romi) ambaye ni Mtanzania mtaalam na mwalimu wa ngazi za kimataifa wa karate na Yoga.
Tunapozungumzia watanzania waliozaliwa na vipaji na kufanikiwa kuvipigania na kuviendeleza vipaji hivyo hadi kufikia kiwango cha kimataifa jina la Sensei Rumadha Fundi aka Romi hatuwezi kulikwepa
Mtanzania huyu makazi yake ni nchini marekani. Kabla ya kujikita huko yeye alikuwa ni mmoja ya wanafunzi wa karate katika dojo lililopo shule ya Sekondari ya wasichana ya Zanakaki jijini Dar es salaam chini ya mwalimu wake Sensei Natambo Guru Kamara Bomani (RIP). Baada ya hapo Sensei Rumadha akaenda kwa mafunzo zaidi nchini Japan,Sweden na Denmark. Pia akachaguliwa kwenda nchini India kwa mafunzo ya kuwa mtaalamu wa Yoga,
Kwa vipaji hivi vya Karate na Yoga vya ngazi ya kimataifa, Sensei Rumadha Fundi anaiwakilisha Tanzania kuwa nchi ya wenye vipaji .Sensei Rumadha Fundi ni mwalimu wa karate na yoga
mwenye utalaamu na upeo wa hali ya juu sana,tena mwenye nidhamu.
Sensei Rumadha ni mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii ughaibuni.
Sensei Rumadha ana mkanda mweusi ngazi ya tatu (Black belt 3rd Dan ya mtindo wa Goju Ryu, ambayo ni chimbuko la dojo iliyojengwa na Master Eiichi Miyazato miaka 63 iliyo pita huko mjini Naha, Okinawa baada ya kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu , Master Chijun Miyagi , ambayo hivi sasa inaendeshwa na mtoto wake Yoshihiro Kancho Miyazato. Sensei Rumadha Fundi, kwa sasa ndiye mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" tawi la Tanzania.