Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema watu 13 wenye mitambo ya kufyatua kazi za wasanii za nje na ndani wakutane kituo cha kati wakiwa na nyaraka za kufanya kazi hiyo.
Akizungumza na Wasanii hao pamoja na Wananchi leo katika mkutano wa kupambana na uharamia wa kazi za wasanii , Makonda amesema kuna watu wanafanya kazi za ujanja ujanja kwa kuwanyonya wasanii.
Amesema kuwa kuanzia leo ni mwisho kwa wale ambao wanafanya kazi za kuuza nyimbo za wasanii na wanaotakiwa kufanya hivyo ni wale ambao wenye mikataba na wasanii wenye nyimbo husika.
Makonda amesema kuwa kazi zote za wasanii za zinatakiwa ziwe na sitika za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ili nchi iweze kupata mapato kujenga huduma za wananchi.
Aidha amesema kuwa wauza wa kazi za wasanii mkononi zinatakiwa kuwa na stika za TRA pamoja na kuwa na kibali maalumu cha kumtambulisha kufanya kazi hiyo kutoka bodi ya filamu.
Hata hivyo amesema kuna watu wanafanya kazi za kuwarubuni wasanii na kufanya maisha yao yawe duni katika kazi hiyo wakati Nigeria inaongoza kwa kupata mapato kupitia kazi za filamu.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na Wasanii katika mtaa wa Mafya mara baada ya kumaliza maandamano ya wasanii kupinga uuzwaji wa filamu za nje ambazo zinachangia kushuka kwa thamani ya filamu za ndani kutokana na bidhaa hizo kutolipiwa kodi
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akiwa katika maandamano na wasanii wa Filamu hapa nchini kupinga uuzwaji wa filamu za nje ya nchi ambazo hazilipiwi ushuru.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini(BASATA), Godfrey Mwingereza akizungumza na wasanii wa filamu waliofika katika maandamano hayo yaliyoitimshwa katika mtaa wa Mafia Kariakoo
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Simon Sirro akizungumza na wasaniii hao.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu nchini , Jimy Mafufu akizungumza kwa niaba ya wasanii katika mkutano huo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na Wasanii waolifika karikoo mara baada ya maandamano ya kupinga Biashara ya uuzwaji filamu za nje
Kundi la Wasanii wakishangilia