#BMGHabari
Lile tamasha la burudani la Nyanza Festival 2017, lililopaswa kufanyika hii leo April 16,2017 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza limeahirishwa kwa kile kinachodaiwa kwamba ni aliyepewa tenda ya muziki kuingia mitini.
"Taarifa Muhimu, Tamasha la Nyanza Festival limeahirishwa kutokana na sababu zisizozuilika na litafanyika baada ya wiki mbili yaani 29/4/2017". Amebainisha mratibu wa tamasha hilo, Fabian Fanuel.
Awali Afisa Habari wa Nyanza Festival 2017, George Binagi, alibainisha kwamba zaidi ya wasanii 30 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa tayari wamethibitisha kupanda jukwaa la Nyanza Festival 2017 hivyo niwasihi wapenzi wa burudani wakae tayari kwa burudani hiyo ambapo kiingilio itakuwa elfu tano tu.
Nyanza Festival ni tamasha lililoasisiwa na Wanatasnia mbalimbali kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wanamuziki, watangazaji, waandishi wa habari, Madjz na wadau wengine wengi kupitia umoja wao wa Mwanza.Com chini ya kampuni ya Famara Entertainment, lengo likiwa ni kuukuza na kuuendeleza zaidi muziki wa Kanda ya Ziwa.