Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Viongozi wa Wanyarwanda, Waganda na Wakongo wanaoishi nchini Ubelgiji Wakutana na Balozi Kamala Ofisini kwake mjimi Brussels

$
0
0
Viongozi wa Wanyarwanda, Waganda na Wakongo Wanaoishi Ubelgiji Wakiwasilisha Ujumbe Maalum kwa Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa). Viongozi hao wamewasilisha ujumbe wa wenzao 120 walioandamana leo hadi kwenye Ubalozi wa Tanzania Brussels kupongeza na kuunga mkono ushauri uliotolewa na Mhe. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wa kushauri Serikali za Rwanda, Uganda na DRC kuzungumza moja kwa moja na wapinzani wao kwa nia ya kupata amani ya kudumu katika eneo la Maziwa Makuu (Great Lakes Region).
Kiongozi wa Baraza la Taifa la Mabadiliko ya Demokrasia Rwanda (NCDC) Balozi Munyeshyaka Ildephonse akimkabidhi Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa) ujumbe kwa niaba ya Wanyarwanda, Waganda na Wakongo wanaoishi Ubelgiji ambao wameandamana leo hadi Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji kupongeza na kuunga mono ushauri wa Mhe. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete aliotoa kwa Serikali za Rwanda, Uganda na DRC kuzungumza na wapinzani wao kwa nia ya kupata amani ya kudumu katika ukanda wa Maziwa Makuu. Wanyarwanda, Waganda na Wakongo wapatao 120 wameshiriki katika maandamano hayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>