Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi mikoa ya Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiweka jiwe la msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Mama Janeth Magufuli wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa wakati akielezea kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amechuchumaa kwenye mfano wa Reli ya Kisasa (SGR) na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu Profesa Norman Sigala mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli hiyo, wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na Hawa Ghasia (Mb).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati akipita katika katika ya mfano wa Reli hiyo itakayojengwa. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA