Na Dotto Mwaibale
BARAZA la Uongozi la Dini na Amani Tanzania (IRCPT), limesema ipo haja mchakato wa Katiba Inayopendekezwa kufikia tamati kwa kuwa ina mambo ya msingi kwa Watanzania.
Mkurugenzi wa Baraza hilo, Mchungaji Thomas Godda amesema ni vema viongozi wa dini wakatimiza wajibu wao kwa kuihamasisha Serikali imalize mchakato huo sanjari na kuhamasisha wananchi kusoma Katiba iliyopo ili kuwajengea uelewa mpana.
Ametoa kauli hiyo leo Dar es Salaam kwenye semina ya siku mbili ya kuhamasisha uhiishaji wa Katiba Mpya kwa viongozi wa dini inayoendelea kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam ambayo imeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Aliongeza kuwa viongozi wa dini si wanaharakati bali ni watu wanaotoa uamuzi wao kwa hekima huku wakiaminiwa na wafuasi wao wakiwemo viongozi wa serikali.
Mkurugenzi wa Baraza la Dini na Amani Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Godda, akihutubia wakati akifungua semina ya siku mbili ya viongozi wa dini kuhamasisha uhiishaji wa katiba mpya inayoendelea Hoteli ya Golden Tulip Posta jijini Dar es Salaam leo. Semina hiyo imeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Mwenyekiti wa Taifa wa Wanawake wa Baraza la Kiislam Tanzania (Bakwata), Shamim Khan (kulia), akizungumza katika semina ya siku mbili ya viongozi wa dini kuhamasisha uhiishaji wa Katiba mpya iliyofanyika Dar es Salaam leo. Semina hiyo imeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)