Na .Tamimimu adam- Jeshi la Polisi ,Moshi
Mahakama ya hakimu mkazi Moshi, mkoani Kilimanjaro imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka 67 jela wakiwemo raia wawili wa Kenya na mwanamke mmoja mtanzania baada ya kupatikana na hatia ya kula njama na kupora shilingi million 239 katika benki ya NMB tawi la Mwanga, Kilimanjaro.
Uporaji huo ulifanyika julai 11,2007 ambapo watu hao waliiba bunduki aina ya Sub machine gun (SMG) mali ya Jeshi la Polisi nchini, ikiwemo kuuawa kwa askari Polisi Ex- PC Michael Milanzi aliyekuwa lindo.
Jopo la makakimu watatu wakiongonzwa na Panterine Kente waliwajata washitakiwa hao waliofungwa ni wanaume wawili raia wa Kenya ambao ni Samweli Gitau maarufu kwa jina la Saitoti na Michael Joseph Kimani Pamoja na mwanamke Elizabert Elias marufu kwa jina la bella mkazi wa Kwangulelo mkoani Arusha.
Katika hukumu hiyo, washitakiwa hao walihukumiwa miaka saba kwa kosa la kwanza ambalo ni kula njama, miaka 30 kila mmoja kwa kosa la uporaji pamoja na mika 30 kwa kosa la wizi wa silaha.
Hakimu huyo alisema kuwa adhabu hizo zinaenda pamoja hivyo washitakiwa watatumikia kifungo cha miaka 67 jela, mbali na hukumu hiyo mahakama hiyo pia iliwaachia huru ndugu watatu ni ambao ni Devotha Elias Masenza, Ntibasana Elias Masenza na Julian Elias Masenza na mtu mwingine Calist kanje baada ya kutowakuta na hatia katika mashitaka yote matatu.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo , wakili wa Serikali Tamali Mndeme aliomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia kutenda makosa kama hayo.