Mfalme wa nyimbo za asili nchini Tanzania Costa Siboka akiwa na msanii Atomi Sifa "Senetor" kutoka nchini Kenya anayetamba na wimbo wa Obama wametambiana kuonyeshana umwamba kanda ya ziwa.
Wasanii hao mwaka jana walikutana mjini Bunda mkoani Mara kila mmoja akiwa na ziara yake mfalme Siboka akidhaminiwa na bia ya Balimi Extra na Konyagi na Atomi Sifa akiwa chini ya udhamini wa bia ya "Senetor" wamekutana tena jana mjini Geita wakiwa katika ziara Atomi Sifa anatarajia kufanya show leo tarehe 15/06/2013 katika uwanja wa Mwaitogole na mfalme Siboka anatarajia kufanya show kubwa mjini Geita tarehe 27/06/2013.
Wasanii hawa kwa sasa wana washabiki wengi sana ukanda wa Afrika Mashariki na kanda ya ziwa, Atomi Sifa anatamba na wimbo wa Obama, mfalme Siboka anatamba na wimbo wa Ntemelakatoke na Twisile ambazo kwa sasa zimekuwa ni gumzo kwa mashabiki wa muziki huo nchini Tanzania na Kenya . Baada ya ziara hiyo wasanii hao wamekubaliana kufanya nyimbo mbili, kati ya nyimbo hizo mmoja utaitwa Amani yetu ambao wataimba kwa lugha za makabila ya Tanzania na Kenya.
Mfalme Siboka yuko Kanda ya ziwa katika kusherehekea kundi lake kutimiza miaka mitano na utambulisho wa nyimbo zake mpya, Siboka atafanya show mjini Geita, Ukerewe, Kisiwa cha Ghana na kisiwa cha Ukara kwa udhamini wa KONYAGI, BALIMI EXTRA na CXC Afrika.