Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Rais John Pombe Magufuli alipongia madarakani alitangaza elimu bure kwa shule za msingi na sekondari.
Taasisi ya Haki Elimu ni moja ya taasisi ambayo imefanya utafiti katika swala la elimu na kuja na majibu ambayo yameonesha kuwepo kwa mafanikio makubwa katika swala la elimu bure.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo,Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, John Kalage ametaja kuwa tafiti hiyo imebaini kuwa Sera ya elimu bila malipo imesababisha ongezeko la wanafunzi wa darasa la kwanza hasa kwa shule za msingi.
“kulikuwa na ongezeko la asilimia 43 na asilimia 10 kwa shule za Sekondari ,hali iliyosababisha msongamano madarasani na pia kuongezeka kwa uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi kwa darasa la kwanza hadi kufikia mwalimu mmoja kufundisha wanafunzi 164 kwa wastani badala ya wanafunzi 45 wanaotakiwa” amesema Kalage.
Amesema kuwa utafiti huo ambao ulifanyika Wilaya za Njombe ,Mpwapwa , Sumbawanga ,Kilosa , Korogwe ,Tabora Mjini na Muleba kwa kuhusisha shule 28 na Msingi na 28 za Sekondari.
Mkurugenzi wa Haki Elimu nchini , John Kalage akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa tafiti juu ya mpango wa elimu bure nchini.
Aliyekuwa Mwenyekiti ya bodi ya taasisi ya Haki elimu nchini, Profesa Martha Qorro akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ripoti ya elimu bure iliyofanyiwa utafiti na tasisi ya Haki eleimu nchini
Baadhi ya washiriki wakisikiliza ripoti hiyo kwa makini.