Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 116996

RAIS WA ZANZIBAR, DKT. SHEIN AZINDUA KITUO KIPYA CHA UNUNUZI WA KARAFUU ZSTC - PEMBA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akikata utepe kuzindua Kituo Kipya cha Shirika la ZSTC cha Ununuzi wa karafuu katika Kijiji cha Mgelema leo, Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba akiwa katika ziara ya kikazi,(kushoto) Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la ZSTC Dkt.Said Seif Mzee.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimina na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika Kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Cheke Chake Mkoa wa Kusini Pemba leo,kuzindua Jengo la Kituo ZSTC,ujenzi wa Kituo cha Afya na Umeme kijijini hapo akiwa katika ziara maalum ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake walipokuwa wakipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi,Makaazi Maji na Nishati Mhe,Salama Aboud Talib wakati Dk.Shein alipofika katika kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Chake chake leo kuangalia Umeme kijijini hapo sambamba na kuzindua Jengo la Kituo cha Ununuzi wa Karafuu cha ZSTC
Baadhi ya Mawaziri na Viongozi wengine waliohudhuria katika Uzinduzi wa Kituo Kipya cha Shirika la ZSTC cha Ununuzi wa karafuu katika Kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,wakimsikiliza Waziri wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kuzungumza na Wananchi Kijijini hapo leo akiwa katika ziara ya kikazi
Transfoma Mpya iliyowekwa katika kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Cheke Chake Mkoa wa Kusini Pemba,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake akiwa katika ziara zake za kikazi katika Mkoa wa Kusini Pemba leo alifika katika kijiji hcho kuangalia Umeme kijijini hapo sambamba na kuzindua Jengo la Kituo ZSTC. Picha na Ikulu, Zanzibar.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 116996

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>