Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwapa pole Wananchi wa Kijiji cha Kwagube Kazole walioathiriwa Nyumba zao kutokana na upepo mkali uliovuma Jumapili iliyopita.
Balozi Seif akikabidhi fedha kwa mmoja wa Wananchi walioathirika na Upepo Mkali katika Kijiji cha Kwagube uliotokea Jumapili iliyopita.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimkagua Mkuu wa Mkoa wa zamani Bwana Pemba Juma Khamis alipofika nyumbani kwake Bububu Kijichi kuangalia hali yake kiafya baada ya kupata matibabu nchini India.
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Mjini Magharibi Bibi Johari Akida akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipofanya ziara ya kumkagua hali yake Nyumbani Kwake Mwanakwerekwe. Picha na OMPR – ZNZ.