Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Crispin Prospher Mwombeki wa kampuni ya Ujenzi wa Barabara ya Mecco wakati Rais alipotembelea ukarabati wa barabara ya Chwale (Madenjani) mpaka Mzambarautakao inayojengwa na kampuni hiyo yenye urefu wa kilomita tano (5km) katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya kikazi (kulia) katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Miundombinu Ndg. Mustafa Aboud Jumbe
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto)akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Miundombinu Ndg. Mustafa Aboud Jumbe (katikati) alipokuwa akiangalia mashine ya kutilia lami (PAVER) ya kampuni ya Mecco wakati alipotembelea ukarabati wa ujenzi wa Barabara ya Chwale (Madenjani) mpaka Mzambarautakao inayojengwa na Kampuni hiyo yenye urefu wa kilomita tano (5km) katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, akiwa katika ziara ya kikazi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati)akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya ZECON ya Zanzibar Ndg. Ali Mbarouk Juma (kulia) wakati alipofika Daya Mtambwe Kaskazini Pemba kuangalia hatua za Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kasakazini Pemba,(wa pili kulia)Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Mmanga Mjengo Mjawiri
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akizungumza na Wananfunzi wa Skuli ya Daya Mtambwe alipotembelea Ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali unaojengwa na Kampuni ya kizalendo ya ZECON ya hapa Zanzibar, akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kasakazini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati)akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Rashid Hadid Rashid alipotembelea Ukunjwi katika sehemu ya kupokelewa Umeme unaopelekwa kisiwa cha Fundo, Mkoa wa kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya kikazi. Picha na Ikulu.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA