Mbunge wa Jimbo la Mafia, Mbaraka Dau (kulia) akimuleza jambo, Balozi wa Italia nchini Tanzania, Roberto Mengoni wakati alipotembelea bandari ya Kilindoni, iliyopo katika Kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani. Balozi Mengoni, amefanya ziara ya siku 2 katika kisiwa cha Mafia, ambapo aliweza kutembele bandari ya Kilindoni, soko la samaki, hospitali ya wilaya na shule ya Sekondari Kitomondo.
Balozi wa Italia nchini Tanzania, Roberto Mengoni (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Mafia, Mbaraka Dau (kushoto), walipokuwa katika bandari ya Kilindoni, iliyopo katika Kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani.