Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Waendesha BodaBoda wakabidhiwa leseni Baada ya kuhitimu Mafunzo ya Veta

$
0
0
Na Abdulaziz Video,Nachingwea

Jumla ya Vijana 63 Waendesha Pikipiki na Bajaj (MAARUFU BODABODA)Wilayani Nachingwea wamekabidhiwa Leseni za Udereva baada ya kuhitimu Mafunzo yaliyotolewa na Veta na Kitengo cha Usalama Barabarani baada ya Kuwezesha na Mbunge wa Jimbo hilo Ambae Pia ni Waziri wa Sheria na Katiba,Mathias Chikawe.

Katika kufanikisha zoezi hilo Mbunge huyo pia amesaidia kuwalipia Leseni zenye thamani ya Tshs Milioni Tatu ambapo Vijana 50 wamenufaika na mpango huo ambao utakuwa endelevu katika jimbo hilo.

Mpango huo wa kuwezesha Vijana Hao ni Jitihada za Mkuu wa Wilaya Hiyo Bi Regina Chonjo baada ya kukutana na makundi mbalimbali na kubaini Baadhi ya Changamoto ikiwemo mahusiano mabaya kati ya Polisi wilayni humo na Waendesha Bodaboda hali Iliyokuwa Inachangia Uvunjifu wa AMANI Ikiwemo kutotoa huduma kwa Uaminifu Huku wakiwa ni tegemeo kubwa la Usafiri na Usafirishaji Vijijini Wakiwemo WAGONJWA.
Mmoja ya Waendesha Boda boda akikabidhiwa leseni yake na Waziri wa Katiba NA Sheria,Mathias Chikawe katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Nachingwea.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi REGINA CHONJO akizungumza na Waendesha Boda boda wakati wa hafla ya kukabidhiwa leseni zao mara baada ya kumaliza mafunzo.Wa pili kulia ni Waziri wa Katiba NA Sheria,Mathias Chikawe.
Furaha baada ya kuhitimu mafunzo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles