Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii
Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) imekutana na wadau wake kujadili utekelezaji wa Soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Common Market Protocol 2010) tangu ilipoanzishwa upya mwaka 2010.
Wanachama wa Jumuiya hiyo walingia makubaliano ya pamoja ili kuongeza utengamano ambao ulilenga zaidi kuongeza uhuru wa watu kupita nchi za Afrika Mashariki, Kuongeza uhuru wa kusafirisha Mizigo na Biashara pamoja Uhuru wa Mitaji (Free Movement of Capital).
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika majadiliano hayo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sera – Taasisi ya Sekta Binafsi, Gilead Teri amesema kuwa wamekutana kufanya tathmini kujua changamoto pamoja na uboreshaji katika soko hilo.
Amesema wamekutana kujadili ili baadae kutoa maoni kwa Serikali pamoja na viongozi wa Jumuiya hiyo, pia ni jinsi gani Tanzania inaweza kunufaika zaidi na soko la pamoja.
Katika soko hilo Tanzania inanufaika zaidi kupata Kodi,Wananchi kupata ajira kutokana na soko kubwa, familia kupata kipato pamoja na kukua kwa Teknolojia ya uzalishaji.
Sehemu ya Wadau wa Taasisi ya Sekta Binafsi wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Sera wa TPSF, Gilead Teri.
Mkurugenzi wa Sera – Taasisi ya Sekta Binafsi, Gilead Teri akizungumza na baadhi ya wadau wa Taasisi hiyo juu ya kujadili utekelezaji wa Soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Common Market Protocol 2010) tangu ilipoanzishwa upya mwaka 2010.