Baada ya wadau wa muziki wa dansi kutaka kusikia mdundo wa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni inayongozwa na mwanamuziki Kamanda Ras Makunja uchezwe redioni, nyimbo hizo zimekabidhiwa leo katika studio za CITY FM RADIO 91.1 ya jijini Dar-es-Salaam.
Hivyo basi kutoka sasa wadau wa muziki wa dansi
watapata burudani ya kusikia nyimbo za bendi hiyo iliyojijengea umaarufu wa kimataifa na kuteka nyoyo za washabiki katika majukwaa ya kimataifa.
Ngoma Africa band imedumu katika medani ya muziki kwa takribani miaka 23 tangu ianzishwe mwaka 1993 na kiongozi wake Kamanda Ras Makunja.
pia unaweza kuwasikiliza