Picha na habari na Faustine Rutta
Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu(wa pili) kutoka kushoto akiwa na Viongozi wa Tawi la Kichwabuta lililozinduliwa jana kwa shangwe na nderemo mjini Bukoba.
Tawi hilo limepewa Jina la Kichwabuta kutokana na kuenzi kazi ya Mwananchama maarufu wa Klabu ya Simba MZEE HUSSEIN OMARY KICHWABUTA ambaye alishiriki kikamilifu kama mpenzi na Mwanachama wa Simba katika maendeleo ya Klabu hiyo ya Simba.
Tawi hilo mpaka sasa lina Wanachama 160 waliojiandikisha na taratibu zinaendelea kuhakikisha wanapata kadi za uanachama kulingana na utaratibu wa Klabu.
Tawi linaongozwa na Mwenyekiti Ndugu Priscus Isdory Massawe, Katibu ndg. Fauzu BinaMungu, Mhasibu Ndg. Dickson Ishengoma, Msemaji Ndg. Miraji Kichwabuta na Viongozi wengine ili kuhakikisha wanapata Wanachama wengi zaidi.