Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega akifungua mafunzo ya siku moja kwa Madiwani kuhuisiana na Sheria ya Maadili ya Viongozi Wa Umma.
Kamishna wa Maadili Jaji mstaafu Salome Kaganda akitoa taarifa fupi ya Sekritereti ya Maadili ya Umma kwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya Kilwa.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wakiwa katika mafunzo.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya Ya Kilwa Abdallah Ulega akiwa katika picha ya Pamoja na Kamisshna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda na Madiwani wa Halmashauri ya Wiaya ya Kilwa waliohudhuria mafunzo ya Maadili katika Ukumbi wa Jumba la Maendeleo.
Picha na Habari na Abdulaziz Video -Kilwa.
Madiwani Nchini wametakiwa kutambua kuwa wanajukumu kubwa la kusimamia maadili katika maeneo yao pamoja na Halmashauri kwa kuwa karibu na Wananchi ikiwa pamoja na kutatua kero zinazowakabili badala ya wao kujiona ni sehemu ya Halmashauri pekee.
Akifungua semina ya Mafunzo kwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa kuhusu Sheria na Maadili ya Viongozi wa Umma,Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi,Abdallah Ulega alieleza kuwa ili kudumisha demokrasia na Utawala Bora na kuimarisha imani kwa Jamii ni Vema.
Viongozi kusimamia Utekelezaji wa sheria maadili ikiwa Pamoja na Ujazaji wa Tamko linabainisha na Rasilimali Ulizonazo Aidha Ulega aliwataka Madiwani hao kutoa Maamuzi sahihi kwa kufuata sheria ,Kanuni na taratibu kwa kufuata Miongozo na ikiwa Pamoja na Kubainisha Mali alizonazo kama sheria Namba 13 ya maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 inavyoelekeza.
'Ngd zangu Waheshimwa Madiwani lazima mfahamu kuwa suala la Maadili na Utawala Bora ni jambo linalopewa nafasi ya pekee katika Serikali yetu na ili kufikia mafanikio ni muhimu kwenu kuwa na maadili mema ikiwa pamoja na kuwa karibu na jamii hii itaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bora na watumishi wa serikali wawajibike kwa wananchi na vyombo vya habari visaidie ili jamii nayo iwe katika Uadilifu...Alimalizia Ulega.
Akifunga Mafunzo hayo Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Umma,Jaji mstaafu Salome Kaganda alieleza kuwa Mafunzo hayo yameendeshwa chini ya mradi wa Elimu kwa UMMA Unaofadhiliwa na Shirika la kutoa Misaada la Kimarekani(USAID)na kuwezeshwa na Sekretarieti ya Maadili ya Umma alibainisha kuwa Kuongezeka kwa Halmashauri na Madiwani na kufikia Halmashauri 162 na kuwa na Madiwani 4461 ni Baadhi ya Changamoto kwa kutoweza kuwafikia kutokana na ufinyu wa Bajeti hali iliyofanya Halmashauri hiyo kutopatiwa mafunzo hayo toka mwaka 2006.
'Kwa kumbukumbu zangu semina ya kwanza kwa wilaya ya Kilwa ilifanyika mwaka 2006 na semina ya pili mwaka 2009 hii inamaanisha madiwani waliochaguliwa mwaka 2010 hii inamaanisha kuwa madiwani hao hawajapata uelewa kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwa utoaji wa Tamko la Mali kwa Viongozi wa Umma kwa hiyo naomba Ushirikiano kwa Halmashauri kusaidia kuwezesha utoaji wa Elimu ili kutatia baadhi ya Changamoto isije kutokea Diwani au kiongozi wa Umma akapoteza sifa za kuwa Kiongozi..Alibainisha Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
Kufuatia Mafunzo hayo ya Siku Moja yaliyofanyika katika Ukumbi wa Jumba la Maendeleo wilayani Kilwa Baadhi ya Madiwani akiwemo wa Kata ya Miguruwe,Mitole na Lihimalyao wilayani Humo waliiomba Serikali kubadili Sheria hiyo kwa kuongeza na Watumishi wa Umma kufuatia Kuongezeka kwa Ubadharifu Huku Sheria ya Kutowabana na Kama Viongozi wa Umma huku wakiendelea kijilimbikizia mali muda mfupi baada ya kuanza kazi.