Na Zuena Msuya DSM,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo amefungua mafunzo ya ufungaji wa migodi yanayotolewa kwa wataalam wa mbalimbali wanaoshiriki katika Kamati ya Kitaifa ya ufungaji wa Migodi.
Watalaam hao wanatoka katika Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza wakati wa ufungaji wa migodi nchini.Mafunzo hayo yanatolewa jijini Dar Es Salaam,na Serikali ya Canada kwa siku tano kuanzia 27-31 machi 2017.
Akizungumza wakati wa akifungua wa mafunzo hayo, Dkt. Pallangyo alisema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha wataalamu wa migodi nchini kuwa na uelewa zaidi juu ya hatua zote zinazotakiwa kufuatwa wakati na baada ya ufungaji wa migodi ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza baada ya migodi kufungwa.
Dkt. Pallangyo, alifafanua kuwa, kwakuwa Serikali ya Canada imejikita katika Sekta ya Madini kwa zaidi ya miaka 200, hivyo mafunzo hayo yatawasaidia wataalam wa ndani kufahamu na kujifunza namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza kupitia migodi iliyokwishafungwa katika nchi hiyo ili yasijitokeze hapa nchini.
” Tusiwe watu wa kusoma tu na kufunga migodi, tujifunze kwa vitendo kutoka kwao makosa waliofanya wakati wa ufungaji wa migodi kwa kuwa Canada ipo katika Sekta ya madini kwa zaidi ya miaka 200 na tujirekebishe, ili makosa yaliyotokea kwa yasijirudie katika migodi yetu,” alisisitiza Dkt.Pallangyo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ( kulia) na Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Canada, Sue Steffen,(kushoto) akizungumza wakati wa mafunzo ya kufunga wa migodi yanayotolewa kwa Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi.Mafunzo hayo ya siku tano yanatolewa na Serikali ya Canada jijini Dar Es Salaam.

Washiriki wa mafunzo ya ufungaji migodi ambao ni Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi wakifatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yanayotolewa kwa siku tano jijini Dar es salaam na Serikali ya Canada.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ( katika waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi wakati wa mafunzo ya ufungaji wa migodi yanayotolewa kwa siku tano jijini Dar es salaam na Serikali ya Canada. Kushoto kwake ni Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Canada, Sue Steffen, na kulia kwake ni Afisa Rasilimali Watu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Suzan Kiwelu.