Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117046

WAZIRI MWIGULU AHIMIZA UADILIFU POLISI

$
0
0
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba amewataka maofisa na askari Polisi kote nchini kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu ili kujenga taswira nzuri kwa wananchi wanaowahudumia jambo ambalo litaongeza imani na ushirikiano katika kukomesha vitendo vya uhalifu nchini.
Waziri Nchemba ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua kikao kazi cha Maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kutoka makao makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na vikosi kutoka bara na Zanzibar kinachoendelea mkoani Dodoma.
Alisema Pamoja na Jeshi hilo kufanya kazi nzuri bado linakabiliwa na changamoto ya baadhi ya askari na maofisa wasio waadilifu wanaofanya vitendo vya  kuwabambikia wananchi kesi na wakati mwingine kuwabadilishia kesi ili kujenga mazingira ya kupatiwa rushwa jambo ambalo ni kinyume na maadili ya askari Polisi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu  wakiongozwa na askari wa kikosi cha  bendera kuingia ukumbini  kwa ajili ya ufunguzi wa kikao kazi cha mwaka kinachowahusisha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) akiongea na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu  wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
 Baadhi ya maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi wakiimba wimbo wa maadili ya afisa wa polisi wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa hao na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) akitoa hotuba ufunguzi wa kikao kazi cha mwaka kinachowahusisha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.  Picha Na Hassan Mndeme. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117046

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>