Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage amewataka watumishi wa tume hiyo wazingatie maadili na kanuni za utawala bora ili kutekeleza kwa ufanisi jukumu la Tume katika kukuza na kuimarisha demkorasi na utawala bora nchini.
Jaji Kaijage ameyasema hayo alipoalikwa kuwa mgeni rasmi kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es Salaam.
“Jukumu kubwa la Tume ni kukuza na kuimarisha demkorasi na utawala bora nchini, kwa maana hiyo ni muhimu kwamba watumishi wa Tume wazingatie maadili na kanuni za utawala bora ili kutekeleza kwa ufanisi jukumu hili” alisema na kuongeza kuwa:
“Ni muhimu kwa watumishi wa Tume katika utendaji kazi wao kuepuka vitendo vya ukiukwaji wa maadili kama vile rushwa, upendeleo na au ubaguzi wa aina yoyote katika sehemu ya kazi”
Mbali na hayo, Mhe. Jaji Kaijage aliipongeza Tume kufanikisha uchaguzi mdogo uliofanyika mwezi Januari mwaka huu katika jimbo la Dimani na kata 20 za Tanzania Bara kwa kuufanya kuwa wa amani na utulivu pamoja na changamoto mbalimbali zilizoukabili uchaguzi huo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (aliyesimama) akitoa neno la ukaribisho kwa Mgeni Rasmi wa ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume hiyo Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia kwake) kabla ya kufungua kikao hicho.Kulia ni Katibu Mkuu wa (Tughe) Taifa Bw. Heri Mkunda na kushoto ni Katibu wa Baraza hilo Bi. Rose Malo.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Rose Malo akiwasilisha muhtasari wa kikao kilichopita cha baraza hilo huku Mwenyekiti wa Baraza Bw. Kailima Ramadhani (katikati) na Naibu Katibu Msaidizi Bi Uddy Sadiki wakifuatilia muhtasari wa kikao hicho.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA