Na MatukiodaimaBlog Same
mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamle akiwa katika shamba la Mirungi baada ya kukamata kwa watuhumiwa wakulima wa zao hilo haraamu
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Mhe. Rosemary Sitaki Senyamule ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ameendelea na mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kukamata shamba la mirungi.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa Shamba hilo limekamatwa leo kata ya Vudee, kijiji cha Kisesa wilayani humo pamoja na mtuhumiwa aliyekuwa mmiliki wa shamba hilo.
"Tunaendelea na utekelezaji wa agizo la Rais Dkt John Magufuli la kupambana na dawa za kulevya na mbali ya misako endelevu tumekamata pia miche 1450 iliyokuwa ikimwagilia..... analitunza sana shamba lama kama vile ni la mazao ya chakula"
"Tumewapa siku 2 ndugu zao wahakikishe wameng'oa mirungi hiyo na kuiteketeza" mkuu huyo alisema na kuongezea kwamba bado kazi ya kuwasaka wote wakulima wa bangi, mirungi na Viroba inaendelea
"Watu wamekuwa wagumu sana kuacha hii biashara. Na sisi tutapambana kwa kutolala mpaka mirungi inaisha Ardhi ya Same" alitoa wito kwa wana Same kulima mazao sahihi ya chakula na biashara badala ya kulima bangi na Mirungi ambayo amesema mwisho wake ni jela
Mkuu wa wilaya ya Same Mhe. Rosemary Sitaki Senyamle akiwa na mtuhumiwa mkulima wa Mirungi.
.
