Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua OFA kabambe ijulikanayo kama HATUPIMI Bando itakayowawezesha wateja wake wote nchini kuongea bila kikomo mara tu baada ya kujiunga.
“Airtel HATUPIMI Bando” itapatikana katika vifurushi mbalimbali ikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi vilivyosheheni dakika zisiso na kikomo zinazowawezesha wateja wa Airtel kuongea na kufanya mengi zaidi bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa muda wa maongezi kwa kuwa hakuna kupimiwa dakika za maongezi.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa hii kabambe, Mkurugenzi wa Masoko, Isack Nchunda alisema “ Airtel Hatupimi, sasa Hatupimi dakika zenu za maongezi, tunaleta huduma hizi nafuu kwa kuwa tunaamini katika kuendelea kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa kuwapatia thamani ya pesa zao katika huduma na bidhaa zetu.
“HATUPIMI Bando” itawapatia wateja wetu nchi nzima uhuru wa kuongea na familia, marafiki na wadau wa biashara zao kulingana na aina ya kifurushi mteja alichochagua ikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi bila kujali vifurushi vyao kuisha muda wa maongezi. Kuna vifurushi vya Hatupimi kwa siku vya hadi shilingi 1000/= pia vipo vya wiki kwa shilingi 5000, na vilevile unaweza kujiunga na HATUPIMI kwa mwezi kwa shilingi 10,000/= ili ufurahie huduma yakutopimiwa dakika zako ongea bila kikomo Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (wa pili kushoto) na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako kwa pamoja wakizindua Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati) akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo. Wa (pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako
Wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia) , Niki wa Pili (katikati) na Gnako wakitumbuiza jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ya Airtel ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja Airtel kuongea bila kikomo.
KUSOM ZAIDI BOFYA HAPA