Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Nyirembe Munasa, akisisitiza jambo katika ufunguzi wa Mafunzo ya usimamizi wa Sheria ya Mazingira na Udhibiti wa biashara haramu ya bidhaa zinazoharibu tabaka la Ozoni. Mafunzo haya ya siku mbili yanayafanyika katika Chuo cha Utalii Arusha na yanahusisha washiriki kutoka mikoa ya Arusha, Tanga na Kilimanjaro. Wa kwanza kulia na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Rogathe Kisanga na Bw. Japhet Kanizius Afisa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais.
Sehemu ya washiriki wa Mafunzo hayo kutoka Sekta za mbalimbali wakiwemo Maafisa Forodha, Maafisa Biashara, Polisi, Mahakama, Waendesha Mashtaka, Uhamiaji, Wataalamu wa Mazingira na Vyombo vya Habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi katika kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Nyirembe Munasa.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Nyirembe Munasa (Kulia) akiongea na mmoja wa washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa Sheria ya Mazingira na Udhibiti wa biashara haramu ya bidhaa zinazoharibu tabaka la Ozoni. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi. Rogathe Kisanga. (Picha Na Lulu Mussa).