Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117151

WANAUME NDIO WANAONGOZA KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA UONGOZI NA UTAWALA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Takwimu zinaonyesha kuwa wanaume ndio wengi katika nyanja mbalimbali za kiutawala na uongozi kuliko wanawake hali ambayo inahitajika kuwepo kwa taarifa za wanawake katika masuala kufanyiwa kazi.

Hayo yamesemwa na mtakwimu wa Chuo cha Taifa cha Takwimu, Chiskel Masaki wakati wakitoa ripoti ya uwiano wa takwimu kati ya wanawake na wanaume waliofanyia kazi kutokana na mafunzo waliyopata nchini Swiden kwa ufadhili wa Sida, amesema kunahitaji taarifa za wanawake ili kuweza kuwasukuma washiriki katika masuala mbalimbali kuendana na wanaume.

Chiskel amesema kuwa mafunzo hayo ya mwezi mmoja yalishirikisha nchi tano ambazo ni Tanzania, Uganda, Rwanda, Pakstan pamoja na Bangladesh ambapo baada ya mafunzo walifanya takwimu za uwiano wa wanaume na wanawake kwa kila nchi.

Aidha amesema kuwa kutokana na kufanya takwimu wameweza kuona umuhimu wa kuwa na takwimu mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia nchi kuweza kutatua matatizo likiwemo suala la uwiano wanaume na wanawake ambapo wanaume ndio wanaoneka katika ajira , uongozi pamoja na uatwala.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Sylvia Meku akitoa maada katika katika uzinduzi wa ripoti ya uwiano kati ya wanaume na wanawake leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Ufatiliaji na Tathimini wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela akitoa maada katika uzinduzi wa ripoti ya uwiano kati ya wanaume na wanawake leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Sylvia Meku akikabidhi kitabu kwa Mkurugenzi wa Ufatiliaji na Tathimini wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela katika uzinduzi wa ripoti ya takwimu ya uwiano kati ya wanaume na wanawake leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya wasimamizi wa kusimamia Takwimu zilizofanywa pamoja na watakwimu waliofanya takwimu ya uwiano wa wanaume na wanawake.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117151

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>