

Kiongozi wa Msafara wa Mabalozi hao, Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Balozi Omar Yussuf Mzee akifafanua jambo katika kikao kati yao na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), walipotembelea leo ili kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji zinatolewa na Kituo hicho. ambapo amewataka TIC kuhakikisha wanaandaa maeneo ya viwanda kulingana na uzalishaji unaopatikana katika eneo husika.

Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Matilda Masuka akizungumza jambo katika kikao kati yao na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), walipotembelea leo ili kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji zinatolewa na Kituo hicho.

Mkutano baina ya Baadhi ya Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje na uongozi wa Kituo cha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Cliford Tandari, ukiendelea.

Balozi wa Tanzania nchini Oman, Balozi Abdallah Kilima (katikati) akizungumza katika kikao kati yao na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), walipotembelea leo ili kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji zinatolewa na Kituo hicho.