


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, usiku huu anahudhuria Mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaojulikana kama SADC Double Troika, mjini Mbabane Swaziland. Mkutano ambao unajadili kwa kina hali tete ya usalama katika Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo( DRC) na Nchi ya Lesotho, ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Asasi hiyo.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)