BALOZI wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Richard Lupembe, ameweka wazi kuwa Azam FC ni moja ya timu zinazowatia moyo Watanzania wanoishi nje ya nchi, huku akiipa mkono wa ushindi kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane Swallows ya Afrika Kusini.
Lupembe alitoa kauli hiyo wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
“Kwa kweli nimefarijika sana kwa kuiona Azam FC tena kama nakumbuka mlikuja hapa mwaka jana, mlikuja hapa kucheza na Bidvest nikawa mgeni rasmi na mkono wangu ukawa wa kheri mkashinda, nawahakikishieni nitawashika tena mkono na ninauhakika mtashinda tena,” alisema Lupembe
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Richard Lupembe akiwa pamoja na wachezaji wa Azam wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.alip
Kocha wa Azam ... akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya Jumapili.
Beki wa Kulia wa Azam, Shomari Kapombe akiwa anagombania mpira na Kingue wakati wa mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya Jumapili.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA