Msemaji na Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Andrew Felix Kaweesi pamoja na walinzi wake wawili wameuwawa kwa kupigwa risasi asubuhi ya leo na watu wasiojulikana mita chache kutokea nyumbani kwake, Kulambiro jijini Kampala. Kikosi cha Usalama cha nchi hiyo kimethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Pichani ni Gari alitokuwa akiitumia Msemaji na Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Andrew Felix Kawees.