Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117167

MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA AWALI YA UTEKELEZAJI WA UAMUZI WA KUHAMIA DODOMA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dodoma uhakikishe unaondoa vitendo vya ukiritimba kwa baadhi ya watendaji wa serikali ambavyo vinaweza kusababisha ucheleweshaji au kukwamisha ujenzi wa miji mipya mikubwa mitano ya kisasa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 14-Mar-2017 wakati akifanya mazungumzo na viongozi wa mkoa wa Dodoma baada ya kupokea taarifa ya Kikosi Kazi kilichoundwa na serikali kwa ajili ya kuratibu shughuli mbalimbali za Serikali kuhamia Dodoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ni muda muafaka sasa hivi kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma kujiimarisha na kujipanga ipasavyo katika kupokea wawekezaji wenye nia njema ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali mkoani humo hasa wakati huu ambao serikali inahamia Dodoma.

Ameonya kuwa wawekezaji matapeli kamwe wasipewe nafasi ya kuwekeza Dodoma na ametaka uongozi wa mkoa wa Dodoma kuwa makini makundi hayo ili wasije kuvuruga mipango ya serikali ya kujenga Makao makuu ya kisasa katika Manispaa ya Dodoma.

Makamu wa Rais pia ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dodoma kulinda na kuendeleza maeneo yote yenye uoto wa asili ili yasije yakaharibiwa kutokana na uwekezaji utakaofanyika mkoani humo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Wadau wa mkoa wa Dodoma kwenye mkutano wa kazi ambapo Taarifa ya Awali ya mkoa wa Dodoma na utekelezaji wa uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma iliwasilishwa katika ukumbi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
ZXCCC



Viewing all articles
Browse latest Browse all 117167

Trending Articles