Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala ameitisha kikao na viongozi Dini na mila kuwaomba msaada wa kukemea vitendo vya kishirikina katika mkoa huo. Makala amesema hayo katika kikao chake na Viongozi hao pamoja na wenyeviti wa mitaa na vijiji katika mkoa wa Mbeya.
"matukio ya watu kufukua maiti au kutozika kwa imani ya kuwafuafua hayapaswi kuachwa yaendelee , Biblia na Qurhan imeandikwa kuna kufufuliwa, kuna kiama ,kuna pepo ni baada ya kufa nawaomba mnisaidie kutoa Elimu na mafundisho yenye kuondosha matukio hayo" Amesema Makalla.
Makalla awaomba pia kusaidia serikali katika mapambano ya Dawa ya Kulevya kwa kutoa Elimu na hamasa ya kuelimisha madhara ya dawa ya kulevya.
Amesema Mbeya itangazwe kwa sifa nzuri kama Mkoa unaotegemewa kwa uzalishali wa Chakula, Mkoa wa tatu kitaifa kuchangia pato la Taifa na ni Mkoa unapiga hatua kubwa kimaendeleo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na viongozi wa Dini, viongozi wa mila, na mitaa katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mkapa leo jijini Mbeya.
Baadhi ya viongozi wa dini na serikali za mitaa na mila wakiwa katika ukumbi wa mkapa kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla.
Mkuu wa mkoa wa mbeya Amos Makalla watatu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya mbeya mh.William Ntinika (kushoto) Pamoja na viongozi wa Dini mkoa wa Mbeya.