Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117361

DAR, PWANI KUKOSA MAJI KWA SAA 8

$
0
0
SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), limetangaza kuwapo kwa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Majisafi kwa wakazi wa  jiji la Dar es salaam, pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini kwa wastani wa saa 8 siku ya Jumapili.

Meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, ameeleza sababu ya kuzimwa kwa mitambo hiyo ni kuruhusu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukamilisha kazi ya kuunganisha umeme kwenye mtambo mpya wa Ruvu Juu, ikiwa ni moja ya hatua za maandalizi ya uzalishaji wa maji mapya baada ya upanuzi wa mtambo huo.

“Kutokana na Matengenezo hayo yatakayofanywa na Tanesco yatapelekea ukosefu wa huduma ya Maji kwa wakazi wa maeneo ya Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu, Msangani, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba, Kibamba Njia Panda Shule Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, na Luguruni,”.

“Mji Wa Bagamoyo, Vijiji Vya Mapinga, Kerege na Mapunga. Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe” alisema Lyaro.

Maeneo mengine yaliyotajwa ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali Ya Rufaa Muhimbili, Buguruni, Changombe, Keko pamoja na Tabata. 

“Tunaomba wananchi wahifadhi Maji kwa kipindi hiki ili wasipate shida wakati tutakapozima mitambo hiyo”. alisema Bi.Lyaro 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117361

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>