Mkuu wa Wilaya akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maonesho ya bidhaa za kinamama.

Mkuu wa Wilaya akitazama moja ya bidhaa na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na akina mama katika kutengeneza Tanzania ya Viwanda.

Mh. Gondwe akihutubia wananchi siku ya wanawake ambapo alieleza Halmashauri kutoa kipaumbele cha mikopo kwa vikundi vya kinamama na kulinda watoto wa kike kuhakikisha wanamaliza masomo yao bila kukwamishwa.

Mkuu wa Wilaya Mh. Gondwe akajumuika kucheza na kinamama kusherehekea sikukuu yao.![]()
Moja ya kikundi cha kinamama wakipokea cheti cha utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Wilaya.

Moja ya kikundi cha kinamama wakipokea cheti cha utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akisoma moja ya bango la wanawake wa kikundi cha Umoja ni nguvu linaloonesha taswira ya mama aliebeba mtoto mgongoni, kichwani kabeba kuni na jembe na mkononi akiwa amebeba chakula huku mwanaume akiwa ameketi nyumbani kumngoja mama alietoka shamba aje kuandaa chakula.
Picha na Alda Sadango,Afisa Habari,wilaya ya Handeni