Kaimu Mkurugenzi Mipango,Miradi ya Maendeleo na Huduma za Utalii TANAPA,Dkt.Ezekiel Dembe akijibu changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiulizwa na washiriki wa Warsha ya TANAPA na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusiana na mada zilizohusu masuala ya utalii ndani ya hifadhi za Wanyama na Miradi ya ujirani mwema.Warsha hiyo ya siku nne iliyofunguliwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki inaendeleo leo ikiwa ni siku ya pili katika ukumbi wa mikutano wa Siasa na Kilimo,Manispaa ya Iringa mkoani Iringa.Warsha hiyo imebeba kauli mbiu inayohusu wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za Taifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ubunge Ardhi,mazingira na Maliasili,Mh James Daudi Lembeli akifafanua jambo mbele ya washiriki wa Warsha ya siku nne ya shirika la Hifadhi ya Mbuga za Taifa (TANAPA) na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali kwenye mada mbili zilizohusu masuala ya utalii ndani ya hifadhi za Wanyama pamoja na Miradi ya Ujirani mwema.Warsha hiyo imebeba kauli mbiu inayohusu wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za Taifa, unaoendelea kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo,Ofisi za Manispaa ya Iringa,Mkoani Iringa.
Waziri Kivuli (kambi ya Upinzani) Wizara ya Maliasili na Utalii,Mh Mch.Peter Simon Msingwa akichangia kwenye moja ya mada iliohusu Masuala ya utalii ndani ya hifadhi za Wanyama,kulia kwake ni Mkurugenzi wa TANAPA,Bwa.Allan Kijazi na shoto ni Dkt.Ayoub Rioba.
Mmoja wa Wahariri,Charles Misango kutoka gazeti la Tanzania Daima akiuliza swali kwenye warsha hiyo mapema leo asubuhi.
Mmoja wa Wahariri wa gazeti la The Guardian on Sunday,Rodgers Luhwago akiuliza swali kwenye moja ya mada ya leo iliyohusu Masuala ya Utalii ndani ya hifadhi za Wanyama,mapema leo asubuhi.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha hiyo ya siku nne wakifuatilia kwa makini yanayojiri ukumbini humo.