Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo mchana jijini Dar kuhusiana na maendeleo ya maandalizi ya tamasha la pasaka linatlotajia kuanza hivi karibuni.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
Tamasha kubwa la muziki wa injili linalofahamika kama "Tamasha la Pasaka" sasa kufanyika katika uwanja wa Uhuru april 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mratibu wa Tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na sasa uwanja wa uhuru ndio sehemu maalum ya kufanyia Tamasha hilo.
“Malengo ya tamasha la pasaka ni yaleyale ni kuliombea taifa na kumuombea Rais wa nchi Dkt John Pombe Magufuli ili aendelee kutawala kwa amani katika taifa hili” amesema
Ametaja kuwa tamasha hilo kwa sasa litatembea katika mikoa kumi na kufanya uzinduzi wa albamu mbili