Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imewafaidisha zaidi ya wakazi elfu kumi na nne waishio katika vijiji vya Lushoto na Bumbuli kwa kuwapatia mawasiliano ya uhakika kupitia ushirika wao na mfuko wa Maendeleo wa mawasiliano kwa wote UCSAF yaani Universal Communication Services Fund.Uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa Airtel katika kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga, umekuja ikiwa ni wiki moja toka Mfuko wa maendeleo wa Mawasiliano kwa wote na Airtel walipozindua minara mingine mitatu mkoani Dodoma.
Meneja Mauzo wa Airtel Tanga John Nada alisema "Airtel tumejipanga kuendelea kutoa mawasiliano ya uhakika hasa kwa kipindi hiki ambacho TCRA wamezindua huduma ya kuwawezesha wateja kuhama mtandano akiwa na namba ileile ikiwa hawapati huduma nzuri na za uhakika, hivyo basi kwa wakazi wa Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre Airtel ndio mtandao wenu wa ukahika kwa sasa”
“Tunawaomba wakazi wote mtumie fursa hii ya mawasiliano kwa kuwa wabunifu zaidi, tumumieni huduma ya Airtel Money kwa kuwa pia mko mbali na huduma za kibenki tumeni na kupokea pesa ili kuboreshe kilimo kwa kutumia mawasiliano haya ya uhakika toka Airtel” alisisitiza Bw, Nada
Kauli ya wananchi juu ya tatizo la mawasiliano zilithibitishwa na diwani wa kata hiyo ,Mh Edwin Mahunda kwamba wakazi wa Kata hiyo walikuwa wakipanda juu ya miti na kwenye vilele vya milima wakitafuta mawasiliano ili kufanya mawasiliano ya kibiashara na mambo mengine ya kijamii.
“Tunawashukuru sana Airtel na UCSAF kwa jitihada zao za kutuletea mawasiliano, mawasiliano haya yatasaidia wakazi wa hapa kijijini na pia yatawasaidia wanaishio mbali na hapa ili kuweza kufanya shughuli zao vyema, awali hali ilikuwa mbaya sana, ilikuwa huwezi kupiga simu mpaka ufike sehemu yenye muinuko” alieleza Mh Mahunda-Diwani.
Diwani wa kata ya kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda pamoja na Meneja mauzo wa Airtel Tanga John Nada wakikata autepe kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga vikiwemo Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre . Airtel mwaka huu imeanzisha kampeni hiyo na UCSAF ili kupanua mawasiliano katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mawasiliano.
Vifijo baada ya uzinduzi wa mnara huo
Diwani wa kata ya kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda akiongea na wananchi waliojawa na furaha baada ya uzinduzi wa mnara huo.
Mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga vikiwemo Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre . Airtel mwaka huu imeanzisha kampeni hiyo na UCSAF ili kupanua mawasiliano katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mawasiliano.
Diwani wa kata ya kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda pamoja na Meneja mauzo wa Airtel Tanga John Nada wakiwa katika picha ya pamoja na baasdhi ya wananchi baada ya kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga