Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117380

Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha mkoani Pwani

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli ametengua rasmi nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Shirika Elimu Kibaha Dkt. Crispin Mpemba ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za kiutendaji zinazomkabili.

Akijibu swali la Waandishi wa Habari waliotaka kupata ufafanuzi juu ya hatma ya tuhuma mbalimbali zinazolikabili Shirika la Elimu Kibaha ambazo zimekuwa zikiandikwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa, Mhe. Simbachawene alisema kutokana na kuwepo kwa tuhuma mbalimbali za uendeshaji, Mhe. Rais Magufuli tarehe 4/3/2017 ametengua rasmi nafasi ya Mtendaji huyo ili kupisha uchunguzi.

“ Ni kweli tuhuma juu ya uendeshaji wa Shirika la Elimu Kibaha likiwemo suala la Mikataba iliyoingiwa na Shirika hilo zimekuwepo kwa muda mrefu sasa. Sisi kama Wizara hatukutaka kukurupuka kufanya maamuzi na tukaamua kuunda kikosi kazi ili kufanya uchunguzi na matokeo ya uchunguzi huo yanapelekea kuwepo kwa hoja zinazohitaji uchunguzi zaidi. Hivyo, ili uchunguzi huo uweze kufanyika Mhe. Rais amemsimamisha kazi Mtendaji huyu Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yake. Alisema Mhe. Simbachawene

Alisema uamuzi wa kumsimamisha umechukuliwa kwakuwa tuhuma za awali zilizojitokeza dhidi yake zinajenga hoja ya kuhitajika kufanyika kwa uchunguzi zaidi.

Kwasasa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha inakaimiwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117380

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>