Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117380

MPINA AMTAKA MKANDARASI WA UJENZI WA UKUTA WA MTO PANGANI KUMALIZA KWA WAKATI

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina, amemtaka kandarasi anaeshughulika na ujenzi wa ukuta wa mto Pangani kampuni ya ( DEZO CIVIL CONSTRUCTION L.TD ) kukamilisha ujenzi wa ufukwe wa huo kwa kipindi cha muda wa miezi kumi.

Ujenzi huo wa sehemu ya ufukwe wa kaskazini ambao una urefu wa mita 950 ambazo kati yake mita 550 zipo katika ujenzi wa awali utagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 2.4, unafadhiliwa na Mfuko wanchi maskini zaidi duniani LDCF kupitia shirika la kimataifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira UNEP na serikali ya Tanzania, kwa usimamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.

Aidha, Katika ziara yake ya kutembelea utekelezaji wa miradi wa kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi katika fukwe za mto pangani leo Mkoani Tanga, Naibu Waziri Mpina amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo hayo ya mto pangani kuhepuka uharibifu wa mazingira ya ufukwe huo kwa kupanda miche ya miti ya mikoko ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo wa kuhifadhi fukwe ya mto Pangani, na kuwaasa kuhepukana na shughuli za kibinadamu ambazo si rafiki kwa mazingira hayo ili kunusuru fukwe hiyo kuliwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi Zubeda Abdalah Amemuomba naibu Waziri Mpina Kuiangali kwa jicho ya pekee fukwe iliyoko katika maeneo ya Tanga DECO ambayo imeathirika kwa kiasi kikubwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabia nchi na haipo kabisa katika bajeti na mchakato mzima wa kunusuru fukwe..”utafutiwe ufumbuzi kupitia serikali au taasisi za kimataifa ili kuweza kuinusuru.” Alisema Mkuu wa Wilaya.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewasa wasimamizi wa mradi huo kutumia fedha husika kwa matumizi kusudiwa kama vile mafunzo ya upandaji, utunzaji na uendeleezaji wa mikoko kwa wana vikundi kwani imezoeleka huko nyuma kuwa fedha kama hizo zimekuwa zikitumika kwa matumizi yasiyo kusudiwa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Pangani Bw. Sabas Chambas, amewataka wadau wa maeneo yote ya Pangani wasimamie na kutunza miti ya mikoko kuchukua taadhari kwa kuzingatia athari za kimazingira kupitia wataalam kutoka wakala wa Taifa wa misitu TFS, na Serikali ya Wilaya. Awali imeelezwa kuwa, serikali ipo katika mpango wa kutafuta fedha, kwa ajili ya ujenzi wa fukwe ya kusini mwa mto pangani.

Mradi huo wa unaofadhiliwa na mfuko wan chi maskini zaidi duniani unahusisha, ujenzi wa kuta za fukwe ya mto pangani, Kisiwapanza Pemba na Kilimani Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela akizungumza na Naibu Waziri Mpina na Ujumbe wa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Merdad Kalemani haupo Pichani, katika ziara za ma Naibu Waziri hao Mkoani Tanga., kulia ni Msaidizi wa katibu tawala wa mkoa wa Tanga, Bi. Monica Kinara.
Afisa misitu wa Wilaya ya Pangani Bw. Twairu Mkongo akielezea jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri Mpina katika fukwe ya mto Pangani.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wsa Rais Mhe. Luhaga Mpina akiongea na wanahabari alipokuwa akihitimisha Ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa ukuta wa mto Pangani ulioathiriwa na athari za mabadiliko ya Tabia Nchi.
Katika Picha ni sehemu ya Fukwe ya Mto wa Pangani iliyoliwa na Bahari. (Picha na Habari zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117380

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>