Na Humphrey Shao, Globu ya jamii
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amewataka wazazi kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kwa kuchangia maendeleo ya elimu.
Kumbilamoto amesema hayo katika mkutano wake na wazazi wa shule ya Msingi Miembeni kata ya Vingunguti .
“lazima niwambie ukweli, hili suala la elimu bure limetusaidia sana katika kata yetu ya vingunguti, hivyo ni vyema kila mtu akawa na wajibu wa kuchangia angalau kidogo katika maendeleo ya elimu kama sadaka ili watoto wetu waishi katika mazingira mazuri” amesema Kumbilmoto.
Kumbilamoto ametolea mfano uwepo wa mabembea katika shule za msingi katika nchi za falme za kiarabu, ambako alikuwa mapumzikoni hivi karibuni ,amesema shule za vingunguti lazima ziwe na bembea kama za uarabuni.
Aidha amepata kuchangia ndoo mbili za rangi na makopo manne kwa ajili ya kupakwa katika darasa la kwanza .
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Idaya Ndevu mbili alimshukuru Meya huyo kwa msaada wake na kumuomba aendelee na moyo huo huo.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamoto akizungumza na wazazi wa mtaa miembeni katika kikao cha kamati ya shule.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akikabidhi makopo ya rangi kwa kamati ya shule ya msingi miembeni
Baadhi ya Wananchi na Wazazi wakiwa wamekaa kwa makini wakimsikiliza Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala
Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Miembeni,Idaya Ndevumbili akizungumza na wazazi wa shule hiyo