Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117409

SHEREHE YA KUUAGA MWAKA 2016 NA KUUKARIBISHA MWAKA 2017 PAMOJA NA KUAGA WASTAAFU WA JESHI LA POLISI SHINYANGA

$
0
0
Hapa ni ndani ya ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga ambapo usiku wa Ijumaa Machi 3,2017 Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanya sherehe ya kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017 pamoja na kuwaaga wastaafu wa jeshi la polisi. 

Mgeni rasmi katika sherehe hizo ambazo zimehudhuriwa na maafisa wa polisi,wakaguzi,askari wa vyeo mbalimbali na wadau wa usalama alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack. 

Akizungumza wakati wa sherehe hizo Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro alisema Machi 3 kila mwaka huwa ni siku ya Polisi ‘Police Family Day’ ambapo pamoja na kuadhimisha siku hiyo,jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limeamua kuwafanyia sherehe ya kuwaaga wastaafu 10 wa jeshi hilo sambamba na kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017. 

“Tumeanza sherehe hizi kwa mkuu wa mkoa kukagua gwaride katika uwanja wa Shycom lakini pia kutoa tuzo kwa askari na wadau waliofanya kazi vyema mwaka 2016 katika ulinzi na usalama wa mkoa wa Shinyanga”,alisema kamanda Muliro. 

Naye Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack alitumia fursa hiyo kulipongeza jeshi la polisi mkoani humo kwa kuendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama na sasa vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu wenye ualbino yamepungua kwa kiasi kikubwa. 

Mwandishi wetu,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa sherehe hizo ametusogezea picha 65 za matukio yaliyojiri ukumbini 
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiwa ameshikilia kisu kabla ya kukata keki.Wa pili kutoka kulia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo Elias Mwita 
Ijumaa Machi 3,2016 katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga-Aliyesimama ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza wakati wa kufungua sherehe ya kuwaaga wastaafu wa jeshi la polisi na kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.Kulia ni mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.Kushoto ni mke wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mama Muliro 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwaomba wadau wote wa ulinzi na usalama kuungana na jeshi la polisi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kuimarisha amani ya mkoa wa Shinyanga 
Wadau wakiwa ukumbini .


Viewing all articles
Browse latest Browse all 117409

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>