Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117409

MD KAYOMBO: YALIYOPITA SI NDWELE TUGANGE YAJAYO

$
0
0
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amewataka wenyeviti wa Mitaa iliyopo katika Manispaa hiyo kutumia vyema nafasi zao za uongozi kwa kuwatumikia wananchi kwa haki huku akiwasihi kuishauri serikali katika majukumu yake ili kuwa na maendeleo chanya katika maeneo yao sawia na kupunguza lawama za mambo yaliyopita ili kuwa na Manispaa imara yenye ukusanyaji mzuri wa mapato.

MD Kayombo amewasihi wenyeviti hao kuwa na mahusiano mazuri baina yao na maafisa watendaji wa Mitaa kwani kufanya kazi kwa Ushirikiano na Upendo ndio silaha pekee ya kuimarisha utendaji na ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika Mitaa.

MD Kayombo ameyasema hayo Wakati wa kikao cha kazi pamoja na wenyeviti wa Mitaa kilichokuwa na dhamira ya kushauriana namna bora ya kuimarisha mapato ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ili kuwa na uchumi imara, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa hiyo Mtaa wa Kibamba CCM na kuhudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa atazuru kata hadi Kata ili kubaini wapi kumwepwaya na kipi kipaombele katika maeneo husika ili kuanza nayo katika kuimarisha maendeleo ya wananchi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Aliyesimama) Boniface Jacob akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo, Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo na kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Ramadhan Kwangaya
Wenyeviti wakisikiliza kwa makini maelekezo mbalimbali wakati wa kikao cha kazi kilichoendeshwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mhe Boniface Jacob ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Picha zote na Nassir Bakari).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 117409

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>