Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117409

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KUJADILI UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA ISTANBUL KWA NCHI ZILIZO KWENYE KUNDI LA NCHI MASIKINI DUNIANI KWA UPANDE WA AFRIKA

$
0
0
Tanzania imeshiriki katika Mkutano ulioitishwa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya Nchi Masikini Duniani kushiriki katika Mkutano wa kujadili utekelezaji wa Programu ya Istanbul (Istanbul Programme of Action - IPOA) kwa nchi zilizo kwenye kundi la nchi masikini barani Afrika. Mkutano huo umefanyika kwenye Hoteli ya Radisson Blu, Dakar, Senegal kuanzia tarehe 28 Februari hadi 1 Machi 2017.

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Mhe. Bi. Maria Leticia Sasabo, Katibu Mkuu (Sekta ya Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Wajumbe wengine waliohudhuria Mkutano huo ni Bw. Jestas A. Nyamanga, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa , Injinia Nikusubila Maiko ; Mtaalamu wa Masula ya Mkongo Mawasiliano na  Bw. Abilah Hassan Namwambe, Afisa Mambo ya Nchi za Nje, anayeshughulikia masuala ya Kundi la Nchi Masikini Duniani kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “Kufanikisha utekelezaji wa Programu ya Istanbul ndani ya mustakabali wa Ajenda 2030 ya Maendeleo Endelevu” (Accelerating the implementation of the Istanbul Programme of Action within the Context of the 2030 Agenda: A focus on broadband connectivity).

IPOA ilizinduliwa na Jumuiya ya Umoja wa Mataifa mwaka 2011 kwa lengo la kumaliza tatizo la umasikini kwa nchi zinazoendelea ifikapo mwaka 2020. Hadi sasa, Mpango huo unakaribia kuisha muda wake lakini tatizo la umasikini bado ni kubwa na pia idadi ya nchi zilizo kwenye kundi la nchi masikini duniani imeongezeka badala ya kupungua.
Katika Mkutano huo, Wajumbe kutoka nchi mbalimbali Duniani, wamejadili masuala ya matumizi ya Mkongo wa Mawasiliano ya Mtandao “BroadBand Connectivity”, kama nyenzo muhimu ya kuleta maendeleo.

Mkutano huo uliowakutanisha viongozi wa Mataifa mbalimbali na wadau wa maendeleo wamejadili na kuweka mikakati mipya ya namna bora ya kufanikisha na kuharakisha utekelezaji wa malengo yaliyoazimiwa kwenye IPOA. Aidha, Mkutano huo umeainisha  matokeo ya utafiti uliofanywa kuhusu matumizi ya Mkongo wa Mawasiliano katika nchi za Rwanda na Senegal.

Vilevile, matokeo ya Mkutano huo yatazingatiwa kama maoni katika Jukwaa la Ngazi ya Juu la Kisiasa, High Level Political Forum litakaloitishwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na Jamii (Economic and Social Council) litakapofanya mapitio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ifikapo Julai, 2017.

Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi chache zilizopiga hatua kubwa sana katika kuwaletea wananchi wake Maendeleo hasa katika sekta ya Mawasiliano. Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Huduma za kifedha, na za kibenki kwa kutumia mitandao na simu za mkononi na gharama ndogo za huduma za simu na kimtandao ni baadhi tu ya maeneo ambayo Tanzania inaongoza kwa kufanya vizuri.

Mhe. Mama Maria Leticia Sasabo, Katibu Mkuu (Sekta ya Mawasiliano), Wizara akifuatiwa na Bw. Jestas A. Nyamanga Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wajumbe kutoka nchi nyingine wakifuatilia mada mbalimbali katika Mkutano huo.
Bw. Abilah Hassan Namwambe, Afisa Mambo ya Nchi za Nje, anayeshughulikia masuala ya Kundi la Nchi Masikini Duniani kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akiwa katika maandalizi ya Mkutano huo.
Injinia Nikusubila Maiko Mtaalamu wa Masuala ya Mkongo wa Mawasiliano akiwasilisha mada katika Mkutano huo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117409

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>