Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi imesaini mikataba yenye zaidi ya Tsh. Bilioni moja na wakandarasi wa Barabara kwa lengo la kuzifanyia matengenezo baadhi ya barabara zilizo chini ya halmashauri hiyo, zikiwa na urefu wa takaribani km 151.
Taarifa ya Afisa habari na mawasilino wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi kwa vyombo vya habari Bw. Ndimmyake Mwakapiso, imetanabaisha kuwa, halmashauri imeingia mikataba na makampuni 11 ikiwa na thamani ya Tsh. Bilioni 01, milioni kumi, laki 05 na elfu tatu miamoja na 24.
Mwakapiso, amezitaja baadhi ya barabara zitakazofanyiwa matengenezo kuwa ni pamoja na barabara ya Kilosa Mufindi matengenezo ya nara kwa mara km12, mpangatazara- Mlimba km 21, Ihalimba- Igomtwa na usokami km 11 wakati ile ya Iramba – Ipilimo itatengenezwa kwa urefu wa km 13.
Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi inamajimbo mawili ya uchaguzi yenye mtandao mzuri wa barabara km 1,000.6 ambazo halmshauri imekuwa ikizifanyia matengenezo ya mara kwa mara ili kuziwezesha zipitike misimu yote ya mwaka kwa kuzingatia kuwa uwepo wa shughuli za viwanda na mazao ya misitu hususani mbao na nguzo husababisha barabara hizo kutumika sana kwani mapema mwezi disemba mwaka jana ilisaini mikataba 10 yenye dhamani ya milioni 500.
Aidha, halmashauri hiyo kupitia Mkurugenzi Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe, ilianzisha utaratibu mpya wa kusaini kandarasi zote kwa uwazi kwa kuandaa hafla fupi ambayo huwakutanisha wakandarasi wote walioshinda tenda na kwa pamoja kutiliana saini kati ya pande zote mbili.
Mwenyekiti wa halmashauri akikabidhi kandarasi zilizosainiwa kwa mmoja wa wakandarasi huku Mkurugenzi mtendaji Profesa Riziki Shemdoe akishuhudia.
sehemu ya wakandarasi 11 wakiwa ofisini kwa Mkurugenzi mtendaji, tayari kwa hafla fupi ya kusaini kandarasi zao, aliyeka mbele ni Profesa Shemdoe Mkurugenzi Mtendaji.