Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Malale Hamsini ameweka wazi kuwa wachezaji walishindwa kuzitumia nafasi za wazi walizozipata katika mchezo wao dhidi ya Yanga na kuambulia kipigo cha 2-0.
Malale ameweka wazi kuwa, hawezi kuwalaumu wachezaji wake kwa kushindwa kutoka na ushindi kwenrye mchezo huo ambapo dakika 45 za kipindi cha pili Yanga walicheza wakiwa pungufu baada ya mshambuliaji wao Obrey Chirwa kutolewa kwa kadi nyekundu.
Amesema , walipata nafasi za wazi ila safu ya ushambulaji haikuwa makini na hata hivyo umakini wa safu ya ushambuliaji wa Yanga uliweza kuharibu mipango yao ya kupata goli.
“Washambuliaji wangu hawakuwa makini kuweza kupata goli kwani Yanga walicheza wakiwa pungufu kwa dakika 45 za kipindi cha pili na zaidi safu ya ulinzi ya Yanga ilikuwa makini kuharibu mipango ya timu yangu,"amesema Malale.
Uwezo wa wachezaji wa Yanga wa mmoja mmoja uliweza kuisaidia kupata ushindi ule ingawa walicheza wakiwa pungufu.