Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

HOJA YA HAJA: MAONI NA ANGALIZO JUU YA RASIMU YA KATIBA

$
0
0
Dear Ankal
Kwa kweli wajumbe wa tume ya katiba wameyatendea  haki maoni ya watanzania  juu ya katiba  mpya. Ingawa  sijapata  muda  wa kusoma  kifungu hata kifungu kwa  utulivu, lakini kwa muonekano wa  awali  rasimu ni  nzuri  na itahitaji marekebisho machache  ya kimsingi.  Rasimu ya  katiba  imependekeza kuwepo kwa  serikali tatu, yaani ya  Muungano, ya Tanzania zanzibar(ambayo ipo kwa sasa) na ya Tanzania Bara( ambayo katika  katiba ya zamani imo ndani ya serikali ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania). Kwa  utaratibu wa tume rasimu ya katiba itajadiliwa katika mabaraza mbalimbali yalioundwa katika ngazi tofauti na baadae kwenye  bunge la katiba  na mwishowe itapigiwa kura ya maoni na itakuwa tayari mwaka 2014. Serikali , inataka   katiba hii ianze  kutumika katika uchaguzi wa mwaka 2015.
 
Angalizo langu:
Iwapo  katiba hii  itapita katika mchakato mzima na ikakubalika kwa wananchi kwamba  tuwe na serikali tatu. Serikali  ya Muungano itakuwa na katiba, Serikali ya Tanzania Zanzibar  wanayo katiba yao, Serikaliya  Tanzania bara itakuwa haina katiba yake, hivyo basi  tutabidi  tuanze  mchakato mpya  wa kupata  katiba ya serikali ya Tanzania bara mwaka 2014. Hili linaweza  kuchukua muda mrefu na pengine kuchelewesha au  kuhairisha  uchaguzi wa mwaka  2015.
 
Sijui serikali na wanasiasa wanaliangaliaje  hili.
Wadau wa Globu ya Jamii je mna mawazo gani  kuhusu angalizo hili?


Mdau wa KATIBA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>