Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

Maonyesho ya Wurzburg Festival Ujerumani,Yavamiwa na mafuriko ya maji

$
0
0
Jumamosi ya tarehe 1 Juni 2013,katika viwanja vya maonesho ya Wurzburg Festival, Kulikuwa na majonzi na simanzi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha hasara kubwa na kuvunjwa kwa tamasha hilo lililokuwa likisherekea miaka 25.

Habari za uhakika zimevuja kuwa vikosi vya zimamoto na wanausalama viliingiwa na mashaka baada ya wanii wa Ngoma Africa band aka FFU,kutoweka ghafla katika chumba cha kubadilishia nguo (back Stage) na kutojulikana waliko, wasi wasi ulitanda labda watakuwa wamezolewa na mafuriko !

Lakini baada ya masaa kadha watayarishaji waligundua kuwa mkuu wa bendi hiyo field-marshal Kamanda Ras Makunja alikiondoa kikosi chake baada ya makachero wa bendi hiyo maarufu kama "Anunnaki Empire" kumtonya boss wao kuwa eneo la festival sio salama mto ulio jirani wa eneo hilo unajaa maji kwa kasi,Kamanda bila kuaga kawatoa FFU wa Ngoma Africa band katika hali ya usiri na kuwanusuru vijana wake, na simu yake ikazimwa hadi baada ya masaa fulani ndipo ikawashwa na kuwajulisha waandalizi wa onyesho wasiwe na shaka kamanda na kikosi cha Ngoma Africa band wapo salama kambini,kitendo hicho kiliwaacha midomo wazi baadhi ya wadau ! wengine kudiriki kusema kuwa Simba ni Simba.

Wadaku watonya kuwa tamasha hilo lilianza mwishoni mwa mwezi mei siku ya ijumaa 31.Mai 2013 kukiwa na maelfu ya watu na wasanii mbali mbali walioalikwa wakiwamo mkongwe Manu Dibando,Alfa Blondy,Salifu Keita ndio walioanza kufungua dimba, Ijumaa hiyo hali ilikuwa shwari lakini ilipofika jumamosi hali ya hewa ilianza kubadilika kwa mvua na upepo,wasinii wengine wakiwa kwenye vyumba vya kujitayarishia miongoni mwao wakiwamo "Ngoma Africa band " a.k.a FFU Ughaibuni, baada ya hali ya hewa kuanza kubadilika kwa upepo na mvua ndio inasemekana kuwa mkuu wa F.F.U Kamanda Ras Makunja na kikosi chake Ngoma Africa band,Kuondoka katika eneo la festival (eneo la hatari) liliokumbwa na maji, katika mazingira ya ajabu. Watonyaji wa habari wamedai kuwa walitoroshwa kwa magari mawili meusi aina ya van yalikuwa na madilisha ya kiza.

Kamanda Ras Makunja kateleza kama nyoka na kikosi chake. Mafuliko hayo yamevamia pia baadhi ya miji nchini Ujerumani na ulaya ya mashariki ka kusababisha vifo vya watu 12.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa eneo la tukio
Watu wote walilazimika kuondoka eneo hilo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 115367

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>