Kamera ya Globu ya Jamii,imemnasa Binti huyu ambaye jina lake halikufahamika mara moja katika Maeneo ya Kamata Kariakoo akijitafutia riziki yake kwa kujishughulisha na usafishaji wa Vioo vya Magari ya watu yanayokuwa yamesimama kwenye Mataa ya Kuongozea Magari.Kwa kawaida imezoeleka kuonekana vijana wa kiume ndio wanaoonekana kujishughulisha na kazi hii sehemu kubwa ya jiji la Dar na si wa kike kama alivyoonekana huyu.
↧