Salaam Ankal Michuzi na Wadau wote,
Nimeona mara kadhaa anapotangulia mtu yeyote mbele za haki alimradi ni mtu mashuhuri basi mwili wake hubebwa na GARI LA WAGONJWA.
Sasa kinachonisumbua ni kwanini magari ya kubebea wagonjwa yana bebea maiti.
Je kukitokea mgonjwa atasubiri mpaka hili gari limalize shughuli za msiba ndiyo likamhudumie mgonjwa?
Sikuhizi kuna magari maalum ya kukubebea miili ya waliotutangulia kwenye haki kwanini yasitumiwe hayo. Sijajua hili wazo limetoka wapi ninauliza maana inawezekana kunasababu ya kufanya hivyo, kama kuna sababu naomba tuambiane ili na sisi wengine turekebisha akiba zetu kichwani.
Mdau wa Globu ya Jamii, Uswazi