Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Ushauri kwa Wanyarwanda:Sioni kosa la Kikwete

$
0
0
Na Mzalendo Albert, Arusha

Alichokisema Rais Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa kutafuta amani nchini DRC hakina ubaya wowote, kupelekea Wanyanrwanda wamjie juu na kuanza kumshambulia kwa lugha ambazo hazina ustaarabu kutokana na matamshi yake ya kutaka amani ipatikane kwa mazungumzo.  Pengine kwa kuanza nielezee kwa ufupi alichosema Rais Kikwete ambacho kimesababisha Wanyarwanda wanatahamaki kiasi hiki.

Ajenda ya mkutano ilikuwa ni juhudi za kutafuta amani nchini DRC.  Inaeleweka kwamba vikundi vingi vya waasi kutoka nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu vinafanya shughuli zake kutokea DRC.  Vikundi hivyo kwa miaka mingi vimekuwa viki destabilize DRC kwakuwa muda mwingi vimekuwa vikiendesha mapigano ndani ya Congo.  Juhudi za kuvisambaratisha vikundi hivyo kwa njia za mapigano hazijazaa matunda kwa zaidi ya miaka 19 sasa.

Miaka yote, Tanzania imekuwa ni kimbilio la wanyonge Barani Afrika. harakati za ukombozi wa nchi zote kusini mwa Afrika zimefanyikia Tanzania.  Aidha, Tanzania kwa miaka mingi imefanya juhudi za kutafuta amani sio nchini Congo peke yake, bali katika eneo lote la ukanda wa maziwa makuu. Mengi yamefanywa ikiwa ni pamoja na:
1) kuwa msuluhishi katika mazungumzo ya kutafuta amani Rwanda, Burundi
2) Kuwa mwenyeji wa wakimbizi kutoka Rwanda, Burundi, DRC
3) Kupeleka majeshi ya kulinda amani

Kitu kumoja ambacho Tanzania imejifunza katika miaka yote hii, ni kwamba mapigano/vita mara nyingi sio suluhu ya kudumu ya kumaliza uhasama.  Mazungumzo ndio njia bora yenye kuweza kuleta maridhiano.  

Ipo mifano mingi ya matunda ya mazungumzo.  Leo hii kikundi kilichokuwa kinajulikana kuwa ni cha kigaidi nchini Burundi FNL, ni sehemu ya Serikali ya Burundi kwa sababu, wote walitoa nafasi ya mazungumzo.

Vikundi vingi vya kigaidi vya DRC, viligeuka kuwa vyama vya siasa na kushiriki kwenye uchaguzi, kwa sababu vilikubali mazungumzo.

Leo hii DRC inafanya mazungumzo na vikundi vya waasi na vya kigaidi nchini Uganda ili kutafuta suluhu.  Mazungumzo haya yametokana na juhudi za wakuu wa nchi za maziwa makuu ambayo Rwanda ni mjumbe.  Hivi nani asiyejua jinsi gani vikundi hivyo vilivyofanya vitendo vya unyama na mauaji kwa wananchi wasio na hatia? Wameua, wamebaka, wameiba.....wamefanya kila jambo hovu, lakini bado imeonekana busara ya kukaa mezani kuzungumza. 

Ukiachilia mifano ya kwenye ukanda huu, ipo mifano mingine mingi tu nje ya ukanda.

Nothern Ireland
Yaliyotokea Ireland ya kaskazini kila mtu anafahamu. Maelfu ya watu waliuawa kutokana na vitendo vya kigaidi vya IRA.  Lakini mwisho wa yote, Serikali ilikaa nao meza moja, matokeo yake ni amani kupatikana Nothern Irrland.

Msumbiji na Angola
Huko Msumbiji nani asiyekumbuka magaidi wa Renamo walivyoua maelfu ya watu nchini humo. Lakini mwishowe walikaa mezani na Frelimo, amani ikapatokana.   Hata Angola, nani asiyekumbuka Jonas Savimbi alivyoua mamia ya wananchi wasio na hatia. 

ANC na apartheid
Huko Afrika ya kusini nani  asiyejua kwamba maelfu ya watu walipoteza maisha yao kutokana na sera za ubaguzi na manyanyaso ya serikali ya makaburu. Lakini baada ya kuitikia wito wa kuzungumza, leo hii wanaendelea kuishi kama taifa moja.

Wayahudi na wajerumani
Pengine mifano niliyoitoa waweza kusema haifanani na Rwanda,kwa kuwa nchi zile haziku experience mauaji ya kimbari.  Lakini huko Ujerumani, mauaji makubwa yalifanyika dhidi ya Wayahudi.  Kila mtu anafahamu hilo.  Lakini leo hii ndugu wale hawaendelezi uhasama....

Baada ya mifano hiyo, ni dhahiri kabisa kwamba alichoshauri Rais Kikwete ni sahihi kabisa.  Nchi zote za maziwa makuu ambazo zina vikundi vinavyohasimiana navyo, watumie njia ya mazungumzo kama njia bora ya kumaliza uhasama na kutoa fursa kwa wahusika waondoke Congo na kurejea nchini mwao.  

Kwa kesi ya Rwanda...sio kweli kwamba kila mwanachama wa FDLR alihusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Wapo wana FDRL ambao walizaliwa baada ya 1994 na wanaishi uhamishoni  ikiwa ni pamoja na DRC. 

Hivi ni haki kuwajumisha hao kwenye kundi la magaidi waliofanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994?  

Je hatuoni kutoa fursa ya mazungumzo itawawezesha wana FDLR ambao hawakuwa na hatia na wala hawakuwepo mwaka 1994 kupata fursa ya kurejea nchini mwao?  

Na je Rwanda haioni busara ya kutumia njia ya mazungumzo itawezesha kufikia makubaliano na waasi hao wawatoe waliohusika na mauaji ya kimbari wakashitakiwe?

 Kufanya mazungumzo hakumaanishi ni kutoa msamaha, la hasha.  Kufanya mazungumzo ni kuweka mazingira ya kutafuta suluhu ikiwa ni pamoja na kuweka misingi ya kuchukua hatua mbalimbali kwa wahusika.

Wanyarwanda wame overreact na kuwa emotional pasipo kuwa na sababu ya msingi.  Rais Kikwete na watanzania kwa ujumla, ni watu wa mwisho kuwa sympathiser wa wanachama wa FDLR waliohusika na mauaji ya kimbari mwaka 1994 na wale wanaoendeleza mapigano hivi sasa huko DRC kwani athari za vitendo vyao vilitugharimu sana.... kwani sio tu vilikiuka misingi ya utu ambayo Tanzania inaiheshimu na kuipigania siku zote, bali pia ilitugharimu kwa kupokea wakimbizi katika vipindi tofauti. Vitendo vyao bado vinaendelea kutugharimu hadi leo. Uwepo wa majeshi ya Tanzania kulinda amani nchini DRC  ni matokeo ya vikundi vya aina ya FDLR kuvuruga amani nchini DRC.

Ikumbukwe pia Kitendo cha Tanzamia kuwa Mwenyeji wa Mahakama ya Kimataifa ya Kimbari ICTR, ni ushahidi tosha wa namna ambavyo Tanzania haiungi mkono mauaji ya kimbari  yaliyotokea Rwanda, haina huruma kwa wale wote walooshiriki katika mauaji ya kimbari.  


Hivyo, hapa kama kuna mtu wa kuomba radhi, ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda na wanyarwanda wengine wote walio over-react na kumshambulia Rais Kikwete.

Kusoma walivyomsema Rais Kikwete BOFYA HAPA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>