Maandalizi yanafanyika kwa ajili ya kuwakutanisha wale waliosoma Shule ya Mkwawa, Iringa kuanzia mwaka 1965 hadi 2005 kabla ya kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Mkwawa University College of Education (MUCE)
Siku: Jumamosi 22 Juni, 2013
Mahali: Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa (mkabala na IFM)
Mchango: Shilingi elfu hamsini (50,000/-) @ mtu
Mchango huu ni kwa ajili ya kugharamia matangazo katika vyombo vya habari, vinywaji, chakula, ulinzi, mapambo, kukodi viti na meza, mshereheshaji (MC) na PA, live band. Tiketi zitapatikana wiki moja kabla ya siku ya shughuli
Shughuli hii itakuwa ni mwanzo wa kuchangia Chuo cha Elimu Mkwawa (MUCE) ili kuweza kujenga mabweni (hostels) kwa ajili ya wanafunzi
WanaMkwawa tuko wengi na tuna kila fursa ya kujumuika pamoja kukumbushana ya Makongoro na Magembe, Makanyagio na Lumumba, Aggrey na Shaaban Robert!
MUCE wamefungua portal kwa ajili ya Mkwawa Alumni tafadhali jisajili ili kuwa sehemu ya familia kubwa ya Mkwawa http://muce.ac.tz/index.php/alumni-registration
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Kamati ya Maandalizi kupitia: Catherine David
Email: Cathyjeff2001@yahoo.com
Simu: +255 784/15 609 848
Mkeka wa Nguvu kuingia Iringa mjini.
Bustani ya Garden katika Shule ya Mkwawa, Iringa.
Wadau wakipata msosi enzi hizooo